Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya Afrika huku nchi nyingi zikiadhimisha miaka 50 ya uhuru

Leo ni siku ya Afrika huku nchi nyingi zikiadhimisha miaka 50 ya uhuru

Leo ni siku ya Afrika ambayo inaadhimisha pia kuanzishwa kwa Umoja wa Nchi huru za Afrika mwaka 1963 na baadaye kugeuzwa jina na kuwa Umoja wa Afrika.

Siku hii inatoa fursa kutathimini changamoto na mafanikio kwa serikali na watu wa Afrika. Akizungumzia siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema siku hii ina umuhimu mkubwa kwani mwaka huu nchi nyingio za Afrika zinaadhimisha miaka 50 tangu kupata uhuru na hususani mataifa ya Afrika yanayozungumza Kifanransa na Nigeria nchi ambayo ina idadi kubwa ya watu kuliko zote barani humo.

Ameongeza kuwa Afrika ina umuhimu mkubwa na amezitaka nchi za bara hilo kutumia umuhimu huo kuwa na ushirikiano, na kutafuta amani na maendeleo endelevu kwa watu wake. Lakini kwa waafrika wenyewe siku hii ina maana gani? Dr Salim Ahmed salim alikuwa ni katibu mkuu wa Umoja wa nchi huru za afrika kwa zaidi ya miaka kumi.