Uchaguzi wa madiwani waahirishwa Burundi hadi wiki ijayo
Nchini Burundi, uchaguzi wa madiwani ambao ungefanyika leo umeakhirishwa hadi jumatatu ijayo tarehe 24 Mai.
Tume huru ya uchaguzi nchini humo imesema sababu ya kuahirisha uchaguzi ni matatizo ya kiufundi hasa usumbufu wa kuwasilisha upatikanaji wa kadi za kupigia kura za vyama mbalimbali. Ni wananchi milioni tatu na laki 6 wanaotarajiwa kushiriki mchakato mzima wa uchaguzi .
Uchaguzi wa madiwani utakuwa wa kwanza kwenye mlolongo wa chaguzi tano ukiwemo ule wa urais utakaofanyika tarehe 28 mwezi wa Juni mwaka huu. Kutoka Bujumbura,muandishi wetu Ramadhani Kibuga ametuandalia ripoti hii.