Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi wa kidemokrasia kuanza Mai 24 nchini Burundi

Uchaguzi wa kidemokrasia kuanza Mai 24 nchini Burundi

Baada ya uchaguzi wa madiwani uliokuwa umepangwa kufanyika Mai 21 nchini Burundi kuahirishwa sasa tume inasema utafanyika Jumatatu ijayo Mai 24.

Kwa mujibu wa tume siku hiyo kila kitu kitakuwa kimekamilika na wananchi wako tayari kutumia haki yao ya kidemokrasia .

wadadisi wanasema kwa mara ya kwanza nchini Burundi huenda ikandika historia baada ya machafuko kwa utawala uliochaguliwa na wananchi kufuatiwa na na utawala mwingine kupitia tena misingi ya kidemokrasia.Lakini kampeni zimekwendaje? na Umoja wa Mataifa nchini humo wenye jukumu la kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa haki una yapi ya kunena. Sikiliza makala hii.