Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madereva UM kutotumia simu za mkononi wakiendesha magari

Madereva UM kutotumia simu za mkononi wakiendesha magari

Katika sheria mpya ambayo imezinduliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon hapo jana, madereva wote wa magari ya Umoja wa Mataifa hawatoruhusiwa kutuma ujumbe mfupi kwa kutumia simu zao za mkononi wakati wakiwa wanaendesha magari.

Hatua hii ni koboresha usalma wa barabara na kuokoa maisha. Akizungumza na wandishi wa habari mjini New York wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya kimataifa ya kuboresha usalama barabara, Ban amesema tunaona kujitokeza kwa changamoto mpya ya madereva kushughulishwa na simu.

Ameongeza kuwa utafiti unaonyesha kwamba matumizi ya simu za mkononi yanachangia ajali mara nne na katika mataifa mengine takriban asilimia 90 ya watu wanatumia simu wakiwa wanaendesha jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao na wa wengine.