Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya misaada yawe wabunifu kwenye maeneo ya migogoro:ICRC

Mashirika ya misaada yawe wabunifu kwenye maeneo ya migogoro:ICRC

Mashirika yanayoshughulika na majanga la kibinadamu kwenye mapigano ya silaha, ambayo kwa kawaida yanaendelea kwa muda mrefu bila kwisha, yanahitaji kuwa wabunifu katika kuwahudumia watu wanaopatikana kwenye hali hiyo.

Hii ni kwa mujibu ya reporti ya kila mwaka ya kamati ya kimataifa la shirika la Msalaba Mwekundu , ICRC, ambayo imetolewa leo.

Katika hatua yake ya kakugua operesheni zake katika mataifa 80 duniani mwaka jana, ICRC ilibaini kuwa mapigano ya muda mrefu yanachangia kuwepo matatizo chungu nzima yanayohitaji kukabiliana nayo.