Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya pauni yapatikana kwa kunadi kofia kusaidia watoto

Maelfu ya pauni yapatikana kwa kunadi kofia kusaidia watoto

Princess Beatrice, mjukuu wa malkia wa Uingereza anauza kwa mnada kofia yenye utata aliyovaa kwenye harusi ya binamu yake Prince William na Catherine Middleton, ili kukusanya fedha kwa ajili ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto to raise money for UNICEF.

Fedha hitakazopatikana zitatumika kwa kusaidia watoto waioko katika matatizo na vita. Kofia hiyo iliyobuniwa na Philip Treacey, ili kosolewa vikali na vyombo vya habari na mitandao ya mawasiliano ya jamii kuwa ilikuwa ya kipuuzi.

Lakini Princess Beatrice, ambaye ni balozi mwema wa watoto walio katika migogoro ananadi kofia hiyo kwenye mtandao wa Ebay, ambapo imesha fikia pauni 50,000 sawa na dola $80,000.

Katie Morrison, kutoka shirika la UNICEF nchini Uingereza anasema fedha zitakazopatikana zitaokoa maisha ya watoto wengi.

Na ameongeza kuwa fedha hizo zitagawanywa kwa vituo viwili vya hisani ambavyo vyote vinauhusiaka na masuakla ya watoto, kimoja ni Children In Crisis, ambacho kilianzishwa na mama wa Princess Beatrice ajulikanaye kama Duchess of York, kinachosaidia watoto kwa masuala ya elimu hasa Afghanistan na kinafanya kazi kwa karibu na UNICEF na nusu nyingine inakwenda kwa mfuko mama wa UNICEF”