Sababu za watoto kwenda uhamishoni zaainishwa:UNICEF

Sababu za watoto kwenda uhamishoni zaainishwa:UNICEF

Akizungumza kwenye kongamano moja la kimataifa mjini New York, Mkurugenzi mkuu wa shirika la watoto duniani UNICEF Anthony Lake ameainisha sababu zinazowasukuma watoto wengi kukimbilia uhamishoni.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa katika wakati huu ulimwengu unashuhudia wimbi kubwa la watu likihamisha makazi yao toka upande mmoja na kukimbia sehemu nyingine.

Ameeleza kuwa watu wanaokadiriwa kufikia milioni 214 hutoka kwenye maeneo yao na kwenda sehemu nyingi kiasi ambacho ni kilkubwa mno ikilinganishwa na idadi ya watu duniani.

Mkurugenzi huyo ametoa kauli hiyo wakati akifungua kongamano la kimataifa linalojalilia hali ya uhamiaji duniani, kongamano linalofanyika Mjini New York na kuyahusisha masharika 15 ya umoja wa mataifa pamoja na mashirika mengine ya kimataifa.

Kongamano hilo limewaalika wataalamu mbalimbali ambao wanatazamiwa kujadilia mipango mbalimbali jinsi ya kuwalinda wahamiaji hao.