Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika inahitaji mapinduzi ya kilimo kufikia malengo ya milenia

Afrika inahitaji mapinduzi ya kilimo kufikia malengo ya milenia

Ripoti ya teknolojia na ubunifu ya UNCTAD ya mwaka huu inaitaka Afrika kufanya mapinduzi ya kuzingatia mazingira ili kufukia lengo muhimu la milenia la kukabiliana na njaa.

Ripoti hiyo inasema matumizi ya mbinu mbovu za kilimo pamoja na uharibifu mkubwa wa mazingira umezifanya nchi nyingi za afrika zilizopo kusini mwa Jangwa la sahara kuwa katika hatari ya kutotimiza lengo la milenia la kupunguza njaa ifikapo mwaka 2015.

Ripoti hiyo inasema Afrika inahitaji mapinduzi ya kilimo , lakini yasiige yale ya bara Asia na Amerika ya Kusini bali yake yajikite zaidi katika teknolojia na ubunifu hasa kwa wakulima wadogowadogo. Mkurugenzi wa wa UNCTAD ni Supachai Panitchpakdi