Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muungano wa Ulaya na FAO kuwasaidia wakulima nchini Lesotho

Muungano wa Ulaya na FAO kuwasaidia wakulima nchini Lesotho

Muungano wa Ulaya na shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO, kwa kushirikiana na wizara ya kilimo ya Lesotho wanawasaidia wakulima zaidi ya 36,000 nchini Lesotho.

Msaada huo ambao pia unatolewa kwa ushirikiano na shirika la chakula MAFS unawapa wakulima mahitaji muhimu ya kilimo kama mbegu, mbolea na pembejeo. Ongezeko la bei ya chakula na kuporomoka kwa uchumi duniani kumeiathiri pakubwa nchi hiyo na hususani watu milioni 1.9 wanaotegemea kilimo.

Muungano wa Ulaya umetenga euro milioni sita kusaidia kilimo na umeipa FAo euro milioni nne kukabiliana na upungufu wa chakula kwa sasa na siku za usoni nchini humo.