Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP inakutana na wataalamu kutathmini usambazaji wa misaada kwenye matatizo

WFP inakutana na wataalamu kutathmini usambazaji wa misaada kwenye matatizo

Juhudi zinafanyika ili kuhakikisha chakula kinawafikia walengwa katika maeneo yanayokabiliwa na majanga ya asili au mazingira ya vita.

Maeneo hayo ni kama Haiti, Afghanistan na Somalia. Leo shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP mjini Rome linakutana na wataalamu kutoka Nyanja ya biashara, misaada ya kibinadamu na majeshi, ili kupata suluhu ya mfumo ulio bora zaidi wa kusambaza misaada, kuidhibiti na kuepuka hatari.

Akizungumza katika mkutano huo mkurugenzi mkuu wa WFP Josette Sheeran amesema lengo lake ni kuhakikisha kwamba WFP ambayo inatoa matumaini ya maisha kwa watu takribani milioni 100 kwa mwaka inatimiza wajibu wake ipasavyo na kwa wakati.Akizungumzia suala hilohilo msemaji wa WFP Gregory Barrow amesema kukutana na wataalamu ni fursa nzuri kwa shirika lao.