Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mataifa yaafikiana kupambana na taka za sumu kwa muda maalimu

Mataifa yaafikiana kupambana na taka za sumu kwa muda maalimu

Mkutano wa kimataifa unaojumuisha serikali mbalimbali mjini Geneva umekubaliana kuwa na mpango wa miaka kumi wa kukabiliana na usafirishaji wa takataka za sumu baina ya mataifa.

Wawakilisha 300 kutoka mataifa 90 wamekuwa wakijadili takataka za sumu ikiwemo jinsi ya kukabiliana na takataka za meli nazile zitokanazo na kompyta, simu za mkononi na vifaa vingine vya umeme.

Msemaji wa Shirika La Umoja wa Mataifa la kushughulikia mazingira( UNEP) Julie Marks amesema mkutano huo umepiga hatua katika kuhakikisha kuratibiwa kwa mkataba wa kutengeneza vitu vya manufaa kutokana na takataka za meil.