Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Filamu ya mfuko wa kimataifa kuzinduliwa leo, Ban ni miongoni mwa washiriki

Filamu ya mfuko wa kimataifa kuzinduliwa leo, Ban ni miongoni mwa washiriki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na balozi mwema wa mfuko wa kimataifa (Global Fund) Bi Carla Bruni Sarkozy, mfadhili wa kimataifa Bill Gates, Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan na mwanamuziki wa rock Bono wameungana kupigia debe mfiko wa kimataifa katika filamu iitwayo Global Fund itakayotoka leo.

Filamu hiyo inaonyesha mafanikio makubwa yaliyopatikana kupambana na magonjwa matatu tangu kuanzishwa kwa mfuko huo mwaka 2002.

Katika filamu hiyo Katibu Mkuu wa zamani Kofi annan anatafakari kuhusu ndoto ya awali wakati wa kuanzishwa kwa Global Fund akielezea wasiwasi wa alipoanzisha mfuko huo na kusema hii vi vita na watu wengi walimbeza wakisema hiyo ni ndoto na anasema alikubali kuwa yeye anapenda ndoto kwani kila kitu huanza kwa ndoto.