Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yapongeza hatua ya UM kushughulikia magonjwa yasiyo ya kuambukiza

WHO yapongeza hatua ya UM kushughulikia magonjwa yasiyo ya kuambukiza

Shirika la afya duniani WHO limepongeza hatua ya mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kuridhia azimio la kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Mkutano huo jana usiku umepitisha azimio la kushughulikia magonjwa kama ya moyo, saratani, matatizo ya kupumua na kisukari , magonjwa ambayo huua karibu watu milioni 35 kila mwaka.

Takribani watu milioni 9 kati ya hao hufariki dunia kabla ya kufikisha umri wa miaka 60. Azimio hilo lina lengo la kuzuia ongezeko la vifo vya mapema vitokanavyo na magonjwa hayo duniani kote.