Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya familia duniani yapiga jicho matatizo ya uhamiaji:15 Mai

Siku ya familia duniani yapiga jicho matatizo ya uhamiaji:15 Mai

Siku ya familia duniani inaathimishwa kesho tarehe Kumi na tano mwezi wa tano na siku hii husherehekewa kila mwaka.Sherehe za mwaka huu zimejikita katika athari ya uhamiji kwa familia ulimwenguni.

Kwenye ujumbe wake wa kuadhimisha siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameseme tofauti ya kijamii na kiuchumi husababisha watu kuhama makwao kutafuta maisha mazuri kwingineko , na kwa minajili hii siku ya kimataifa ya familia mwaka huu itaangazia athari ya uhamiaji kwa familia.

Ban ameongezea kuwa wengi wa watu wanahama makwao kwa sababu za kisiasa, umaskini, ukosefu wa ajira, vita au ukiukaji wa haki zao za kibinadamu. Amezitaka jamii zote kuzingatia uhumimu wa kulinda familia kwa manufaa ya matifa yao.