Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikao cha ngazi ya juu cha tume ya maendeleo endelevu (CSD) kimeanza

Kikao cha ngazi ya juu cha tume ya maendeleo endelevu (CSD) kimeanza

Kikao cha nane cha ngazi ya juu cha tume ya maendeleo endelevu kimeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr Asha Rose Migiro ni miongoni mwa wazungumzaji katika mkutano huo pamoja na wajumbe wengine watano.

Mada kuu zinazojadiliwa kwenye kikao hicho ni pamoja na udhibiti wa uchimbaji wa madini kwa maendeleo endelevu, uongozi bora kwa ajili ya maendeleo endelevu, changamoto zinazokabili taasisi mbalimbali ifikapo mwaka 2012 na kuwawezesaha masikini kupata maendeleo kwa kuzingatia masuala kama makazi, miradi mbalimbali na mazingira.