Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mawasiliano ya tekinolojia yanachangia kufikia malengo ya milenia:WSIS

Mawasiliano ya tekinolojia yanachangia kufikia malengo ya milenia:WSIS

Ripoti ya mkutano kuhusu mawasiliano na teknolojia ya mwaka huu (WSIS) imethibitisha kwamba miradi ya mawasiliano na tekinolojia inachangia pakubwa kufikia malengo ya milenia (MDG\'S) ya kuwaunganisha watu kufikia mwaka 2015.

Ripoti hiyo ambayo hutolewa kila mwaka ,safari hii imebaini masuala matano muhimu ambayo yanahitaji kushughulikiwa na jumuiya ya kimataifa ya maendeleo.

Baadhi ya masuala hayo ni uhusiano baina ya malengo ya milenia na mawasiliano, matumizi ya broadband yatakayochagiza uwepesi wa mawasiliano, kutumiwa kwa mawasiliano katika kukabiliana na majanga, kuunganisha watu kwa njia ya mawasiliano, na masuala ya usalama wa matumizi ya teknolojia.