Nchi zinazoendelea zinataabika kupata soko la samaki wao nje:FAO

26 Aprili 2010

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO limesema nchi zinazoendelea zinapata tabu kufikisha samaki wao katika masoko ya nchi zilizoendelea.

Shirika hilo linasema asilimia 50 ya samaki wote wanaoingizwa na mataifa tajiri wenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 40 wanatoka nchi zinazoendelea, lakini sasa nchi nyingi zinazosafirisha samaki hao zinapata shida kukidhi masharti ya mataifa yanayoagisa samaki hao.

Kuanzia Januari mosi mwaka huu muungano wa Ulaya ambao ndio muagizaji mkubwa wa samaki duniani umetaka uingizaji wote wa samaki uambatanishwe na cheti cha kilichothibitishwa na nchi ambayo chombo chake kilitumika kuvua samaki hao.

Lengo kubwa ni kupambana na uvuvi haramu, usiodhibitiwa na usiojulikana ambao ndio tatizo kubwa , lakini FAO ina sema kukidhi masharti hayo ni kuongeza adha na mzigo mkubwa kwa wasafirishaji na ni changamoto. FAO inasema mapato ya nchi zinazoendelea yatokanayo na kusafirisha samaki nje ni dola bilioni 27 kwa mwaka na watu milioni 45 wameajiriwa na sekta ya uvuvi.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter