Skip to main content

Volkano ya Iceland yachelewesha mpango wa makazi kwa wakimbizi wa Kipalestina

Volkano ya Iceland yachelewesha mpango wa makazi kwa wakimbizi wa Kipalestina

Kulipuka kwa volkani nchini Iceland wiki jana kumechelewesha mpango wa kuwapa makazi kundi la wakimbizi wa Kipalestina wanaotoka Iraq.

Wakimbizi 43 wa Kipalestina wakiwemo watoto wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu katika kambi ya mpakani mwa Iraq na Syria baada ya kukimbia kuawa na kunyanyaswa nchini Iraq.

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema wakimbizi hao ilikuwa wasafiri kwa ndege kutoka Baghdad siku ya jumanne kwenda Paris kupitia Amman Jordan. Baada ya mlipuko wa volkano ndege zote kuelekea Ulaya zilisitishwa na nchi nyingi kufunga anga zao, kwa sababu ya moshi wa volkano hiyo.

Sasa kwa kuwa safari zimeanza tena UNHCR inasema wakimbizi hao hivi karibuni wataweza kuelekea Ufaransa .Ni kundi la karibuni la wakimbizi wa Palestina kufaidika na programu ya Ufaransa ya kuwapa makazi wakimbizi wanaoishi katika hali ngumu au walio na mahitaji ambayo hayawezi kushughulikiwa nchini mwao na wakaamua kuomba hifadhi ya ukimbizi.