Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Barbados imemteua waziri wa zamani wa mazingira kuwania nafasi ya mkuu wa mabadiliko ya hali ya hewa wa UM

Barbados imemteua waziri wa zamani wa mazingira kuwania nafasi ya mkuu wa mabadiliko ya hali ya hewa wa UM

Wadhifa wa kuwa katibu mtendaji wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na mabadiliko ya hali ya hewa unahitaji uwezo na ujuzi wa kisiasa,uelewa na upeo wa elimu na taaluma.

Hayo yameelezwa na waziri wa zamani wa mazingira wa Barbados Elizabeth Thompson ambaye nchi yake imemteua kushika wadhifa wa kuwa mkuu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa cha mabadiliko ya mazingira. Bi Elizabeth amesema anakidhi vigezo vyote hasa kwa kuwa ameshafanya kazi ya mazingira,nishati na mabadiliko ya hali ya hewa.

Senata Thompson amesema kwamba kwa kuwa anatoka nchi zinazoendelea anaelewa fika, uzito wa changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa. Na amekwishawahi kupata tuzo ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP kama mwanaharakati kinara. Tuzo hiyo inajulikana kama UNEP's Champion of the Earth Award.