Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku tatu za tathimini ya WHO ilivyokabiliana na mafua ya H1N1 zimekamilika

Siku tatu za tathimini ya WHO ilivyokabiliana na mafua ya H1N1 zimekamilika

Kamati binafsi ya watalamu waliokuwa wanatathimini jinsi shirika la afya duniani WHO lilivyokabiliana na homa ya mafua ya H1N1 imemaliza siku tatu za mwanzo za tathimini yao.

WHO imekuwa ikikosolewa vikali jinsi ilivyokabiliana na mafua hayo ambayo yamekatili maisha ya watu zaidi ya 17,000. Kamati hiyo inayojumuisha wataalamu 29 haitochunguza tuu jinsi WHO ilivyokabiliana na mafua hayo bali itatathimini utendaji wa sheria za kimataifa za afya.

Dr Harvey Fineberg ndiye anayeongoza kamati hiyo akizungumza mjini Geneva amesema wataalamu hao hawako kumshutumu yoyote bali kuangalia funzo lililopatikana na nini kiepukwe siku za usoni.