Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa yuko ziarani nchini Haiti

12 Aprili 2010

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro jana yuko nchini Haiti kwa ziara ya siku mbili.

Tayari ameshakutana na Rais Preval wa nchi hiyo, pia viongozi wengine wa serikali na maafisa wa Umoja wa Mataifa. Asha Rose ametembelea pia moja ya kambi za wakimbizi wa ndani iliyopo Terrain ACRA.

Leo mbali ya kutembelea eneo lililoathirika vibaya na tetemeko la Leogane , atakunata na viongozi wa mashirika ya misaada kupata taarifa ya changamoto wanazokabiliana nazo katika ugawaji misaada ya kibinadamu. Alipozungumza na waandishi wa habari Bi Migiro amesema Umoja wa Mataifa upo Haiti kushirikiana na watu wan chi hiyo kuijenga upya nchi yao.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter