Mkutano wa kimatifa wa ukuaji wa miji na makazi umemalizika Rio de Jeneiro
Mkutano huo uliomalizika Ijumaa Machi 26 umetoka na maazimio mbalimbali likiwemo la kuzisaidia serikali za nchi zinazoendelea kufikia malengo ya miji bora. Miji mingi katika nchi zinazoendelea hususani Afrika haiko katika mpangilio unaofaa, kwani nyumba zimejengwa kiholela na huduma muhimu ni nadra kupatikana au hakuna kabisa.
Tunazungumza na waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi wa Tanzania John Chiligati aliyekuweko kwenye mkutano huo. Waweza kusikiliza makala hii moja kwa moja hapa kwenye mtandao.