Skip to main content

UNAMID yatoa mafunzo kwa wafanyakazi wa magereza Sudan

UNAMID yatoa mafunzo kwa wafanyakazi wa magereza Sudan

Mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika nchini Sudan UNAMID kwa kushirikiana na mpango wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa UNDP na na uongozi wa magereza wa Darfur kaskazini wameanza mpango mpya wa mafunzo kwa wafanyakazi wa magereza na wafanyakazi wa jamii.

Mafunzo hayo ya siku tano yanayofanyika El Fasher yana lengo la kuwapa ujuzi washiriki katika majukumu yao ya kila siku kwa mtazamo wa kuzingatia haki za binadamu, mfano viwango vya kimataifa vya magereza na kuwapa ushauri nasaha wafungwa.

Pia ni katika kuwasaidia wafanyakazi kuwarejesha katika maisha ya kawaida wafungwa na kuwashawishi kuwa watu wanaofuata sheria baada ya kutoka jela.