Skip to main content

ITU kuimarisha mawasiliano zaidi nchini Haiti

ITU kuimarisha mawasiliano zaidi nchini Haiti

ITU imetia saini makubaliano muhimu ya ushirikiano na kampuni ya tekinolojia ya Singapore iitwayo smartBridge solutions ambayo ni mtoaji mkubwa wa huduma ya vifaa vya broadband ili kutoa huduma ya wimax na mfumo wa wiFi kwa lengo la kuimarisha mawasiliano katika kukabiliana na majanga.

Makubaliano hayo yatashuhudia kuwasili na kuanzishwa kwa vituo kumi vya Wimax na ofisi 40 za huduma za vifaa nchini Haiti, ambavyo vitasaidia kuwekwa kwa maeneo karibu 100 ya huduma ya broadband mjini Port-au-Prince na miji mingine iliyoathirika na tetemeko nchini humo.

Mitambo hiyo inategemewa kutoa huduma ya kasi ya simu zisizotumia nyaya na tovuti katika vituo 100 vya wakimbizi wa ndani. Na huduma hiyo itapunguza matatizo ya mawasilino yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi.