Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP na PUMA wametangaza mipango mahsusi wa kushirikiana kusaidia mwaka 2010 wa Bayoanuai (viumbe hai)

UNEP na PUMA wametangaza mipango mahsusi wa kushirikiana kusaidia mwaka 2010 wa Bayoanuai (viumbe hai)

PUMA ambayo ni moja ya makampuni makubwa duniani yanayojihusisha na michezo na Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) wametangaza mshikamano maalumu wa kusaidia viumbe hai duniani na hususani barani Afrika.

Ushirikiano huu waliouita ‘Play for Life' utasaidia mwaka 2010 ambao ni mwaka wa viumbe hai, kuchagiza kuhusu uhifadhi wa makazi na viumbe, miongnoni mwa wapenzi wa kandanda na jamii kwa ujumla wakati wa matukio mbalimbali ya mpira wa miguu duniani ikiwa ni pamoja na mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika yatakayofanyika Angola baadaye mwezi huu na mechi za kirafiki za maandalizi ya kombe la dunia 2010 yatakayofanyika nchini Afrika ya Kusini. PUMA ambayo inadhamini timu 12 za Afrika inatarajiwa kutoa msukumo mkubwa katika mchakato huu wa UNEP. Mwaka wa viumbe hai umezinduliwa na umoja wa mataifa mwaka huu wa 2010 ili kutoa changamoto kote duniani kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mimea, wanyama na mazingira tunayoishi.