UNICEF itaandaa warsha maalumu Copenhagen, kwa watoto kuzingatia mageuzi ya hali ya hewa
Warsha Maalumu wa Watoto Kuzingatia Masuala juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani unaandaliwa kufanyika kwenye mji wa Copenhagen kuanzia Novemba 28 mpaka Disemba 04 (2009), kabla ya Mkutano Mkuu wa UM juu ya Udhibiti wa Athari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa kuanza majadiliano.
Warsha wa Watoto juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa utajumuisha watoto 160 wa kutoka nchi 44 wanachama, wakiwemo vijana wa baina ya miaka 14 mpaka 17, watakaowakilisha mataifa yenye maendeleo ya viwanda na yale mataifa yanayoendelea, halkadhalika.