Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maambukizo mapya ya VVU yateremka kwa 17% duniani - maendeleo zaidi yashuhudiwa kusini ya Sahara

Maambukizo mapya ya VVU yateremka kwa 17% duniani - maendeleo zaidi yashuhudiwa kusini ya Sahara

Ripoti iliotolewa wiki hii bia na Jumuiya ya Mashirika ya UM dhidi ya UKIMWI (UNAIDS) pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO), imethibitisha kwamba ile miradi kinga dhidi ya maambukizo ya virusi vya UKIMWI ndio mipango ilioyawezesha mataifa kuleta tofauti halisi kwenye udhibiti unaoridhisha wa maradhi kwenye maeneo yao.