Pengo la ustawi laendelea kupanuka baina ya mataifa tajiri na maskini, imebainisha kiashirio cha HDI
Kwenye taarifa kuhusu Kiashirio cha Matokeo ya Utafiti juu ya Maendeleo ya Wanadamu, ambacho hujulikana kama Kiashirio cha HDI, iliowakilishwa mapema wiki hii, iliripotiwa kwamba licha ya kuwa nchi nyingi wanachama zilionyesha kuwa na maendeleo ya kiuchumi na kijamii mnamo miaka 25 iliopita, hata hivyo, pengo la tofauti kuhusu ustawi wa jumla, na hali njema baina ya nchi tajiri na nchi maskini, linaendelea kupanuka.
Taarifa ya Kiashirio cha HDI iliotangazwa rasmi Ijumatatu, ni sehemu ya Ripoti ya 2009 juu ya Maendeleo ya Wanadamu, yaani Ripoti ya HDR. Kiashirio cha mwaka huu cha HDI kuhusu ustawi na hali njema ya maisha kwa umma wa kimataifa - hujumlisha kwenye tathmini yake, mchanganyiko wa vipimo juu ya miaka ya mtu anayotarajiwa kuishi, ujuzi wa kusoma na kuandika, uandikishaji wa wanafunzi katika maskuli, na pia makadirio kuhusu Jumla ya Pato la Taifa kwa kila mtu. Utafiti uliendelezwa katika nchi 182. Mwandishi aliyeongoza utayarishaji wa ripoti, Jeni Klugman, alinakiliwa akisema katika miongo ya karibuni "nchi nyingi zilishuhudia vizuizi kadha wa kadha dhidi ya juhudi zao za kukuza maendeleo, kwa sababu ya miporomoko ya uchumi na ile migogoro ihusuyo mifarakano ya kimataifa pamoja na mchanganyiko wa matatizo ya virusi vya UKIMWI na maradhi ya UKIMWI. Mataifa 10 yanayoongoza kimaisha, kwa kuambatana na matokeo ya utafiti kuhusu maendeleo ya ustawi na hali njema kimataifa, awali ni taifa la Norway, likifuatiwa na Australia, Iceland, Kanada, Ireland, Uholanzi, Sweden, Ufaransa, Uswiss na Ujapani. wa wenye wenyewe