Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa 'R2P' wahitimisha mijadala kwenye Baraza Kuu

Mkutano wa 'R2P' wahitimisha mijadala kwenye Baraza Kuu

Baraza Kuu la UM Ijumanne alasiri limekamilisha mahojiano kuhusu lile suala la ‘dhamana ya Mataifa kulinda raia dhidi ya jinai ya halaiki", rai ambayo vile vile hujulikana kwa umaarufu kama ‘kanuni ya R2P.\'

Kwenye hotuba ya kufunga mkutano, Raisi wa kikao cha mwaka huu, cha 63 cha Baraza Kuu, Miguel d'Escoto Brockmann wa Nicaragua aliyaeleza mahojiano kuwa ya hamasa kubwa, makali na yenye mtanuko wa kuridhisha wa mawazo, hali ambayo, alisistiza, haijawahi kuhushudiwa hapo kabla kwenye mijadala ya Baraza Kuu. Juu ya hayo, alisema mataifa bado yana wasiwasi kuhusu hili wazo la ‘kanuni ya R2P' - yaani kanuni inayopendekeza nchi wanachama wa katika UM kuingilia kati, kwa pamoja, kuhami raia ndani ya taifa linaloshindwa kuhami na kulinda umma wake dhidi ya mauaji ya halaiki, makosa ya vita na vitendo vya utakaso wa mila za kijadi. Msimamo wa Baraza Kuu, aliendelea kusema Raisi wa Baraza Kuu, haukuregarega hata kidogo, maana matakwa ya asilimia kubwa ya Mataifa Wanachama yanapendelea kutekelezwa ule mwelekeo wenye kulenga zaidi huduma za kuzuia mizozo isiibuke kwa kushughulikia, awali, vyanzo vinavyosababisha mizozo kujiri. Majadiliano ya kuzingatia ‘kanuni ya R2P' yalianza rasmi wiki iliopita na wajumbe wa kimataifa 94 waliwakilisha maoni na wasiwasi wao. Raisi wa Baraza Kuu anatumai majadiliano ya mada hii kuhusu ‘dhamana ya Mataifa kulinda raia dhidi ya jinai ya halaiki' yataendelezwa zaidi na Mataifa Wanachama katika siku zijazo.