Wataalam wa haki za binadamu ziarani Guyana kuchunguza ubaguzi
Wataalam wa Umoja wa Mataifa wenye asili ya kiafrika watatembelea kisiwa cha Guyaha kuanzia tarehe 2 hadi 9 mwezi ujao wa Oktoba ikiwa ni hatua ya kujifunza hali ya haki za binadamu kwa watu wenye asili ya Afrika waishio katika visiwa hivyo.
Msemaji wa msafara huo Sabelo Gumeze amesema wakati wa ziara hiyo watakusanya taarifa zozoe kuhusiana na ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa kiitikadi na pia ripoti yoyote inayolenga chuki, ili waifanyie tathmini ya ukiukwaji wa haki ya binadamu kundi hilo.
Wataalamu hao watatumia ziara yao kuendelza kampeni ya muongo ya kimataifa wa watu wenye asili wa kiafrika uliotangazwa mwaka 2015 hadi 2024, yenye lengo la kupongeza michango mbalimbali ya watu wenye asili ya kiafrika kwa jamii.
Halikadhalika kuimarisha ushirikiano wa kitaifa, kikanda na kimataifa ili kuhakikisha haki za binadamu za watu wa Afrika wanaheshimiwa, kulindwa duniani kote.
Wataalamu wengine ni Michal Balcerzak na Ahmed Reid ambapo wakiwa huko Guyana watakuwa na mazungumzo na viongozi wa kiserikali, jamii husika, mashirika ya kiraia na pia wanaharakati wa masuala ya ubaguzi wa rangi .