Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanigeria waliokuwa Libya warejea nyumbani kwa wimbo:IOM

Wanigeria waliokuwa Libya warejea nyumbani kwa wimbo:IOM

Zaidi ya wanigeria 150 baadhi yao wakibubujikwa na machozi , waliimba kwa furaha wakati ndege inatua nyumbani Lagos, Nigeria baada ya kukwama Libya kwa miezi mingi wakisubiri kujaribu kuingia Ulaya. Rosemary Musumba na ripoti kamili.

(Taarifa ya Rosemary)

Nats..

Kibao hicho I am coming home.. yaani narudi nyumbani kikiimbwa na raia wa Nigeria wakiwa ndani ya ndege wakitokea Libya…, wanasema ieleze dunia narudi nyumbani na mvua ioshe machungu ya jana.”

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM liliwezesha kurejea kwao nyumbani ambako wengine walisikika wakiimba “Sitoondoka Nigeria tena! Sintosahau asilani nyumbani kwetu!"

Waliimba nyimbo hizo wakati mvua kubwa ikinyesha kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Lagos, na basi lililowabeba uwanjani hapo kuelekea dawati la uhamiaji lilijawa mashamsham.

Miongoni mwao alikuwa Osapolor Osahor alisema "Nina furaha sana, ni kama kushinda bahati nasibu!"

Nats.. Up