Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Akiwa DRC, Katibu Mkuu awaambia viongozi kuachia madaraka

Akiwa DRC, Katibu Mkuu awaambia viongozi kuachia madaraka

Mapema kabla hajaelekea nchini Sudan Kusini,  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewasihi viongozi wa kisaisa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kushiriki mazungumzo jumuishi ya kisiasa kuelekea uchaguzi mwaka huu, na kuheshimu katiba.

Bwana Ban amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari mjini Kinshasa, mwisho wa ziara yake nchini DRC, akieleza wasiwasi wake kuhusu kuchelewa kwa ajenda ya uchaguzi na ripoti za vikwazo dhidi ya vyombo vya habari, asasi za kiraia na vyombo vya upinzani.

Amesisitiza kwamba viongozi wa Afrika na kwingineko hawapaswi kubakia madarakani na kuheshimu udhibiti wa idadi ya muhula wa urais uliowekwa kikatiba.

Aidha amekaribisha kurejeshwa kwa ushirikiano kati ya jeshi la kitaifa la DRC FARDC na vikossi vya MONUSCO katika kupambana na waasi wa ADF, FDLR, na vikundi vingine.