Skip to main content

Dola Milioni 21 kutoka CERF kusaidia Sudan Kusini- Ban Ki-moon

Dola Milioni 21 kutoka CERF kusaidia Sudan Kusini- Ban Ki-moon

Akiendelea na ziara yake barani Afrika, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amewasili Juba, Sudan Kusini akihimiza umuhimu wa kukuza amani na kuacha na mapigano nchini humo huku akitangaza msaada wa dola Milioni 21 kwa ajili ya usaidizi wa kibinadamu nchini  humo. Taarifa zaidi na Amina Hassan

(TAARIFA YA AMINA)

Bwana Ban amekutana na kufanya mazungumzo ya faradha na  Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ambaye kwa mujibu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS rais huyo ameahidi kutekeleza makubaliano ya amani.

Katibu Mkuu amekutana pia na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo na mabalozi, akiwahimiza kuongeza bidii kwa ajili ya amani na usadizi wa kibinadamu ili kupunguza machungu kwa raia wasio na hatia na akaongeza kuwa

(SAUTI BAN)

"Leo natangaza kuwa Umoja wa Mataifa utatoa dola milioni 21 kutoka katika mfuko wetu wa dharura kwa ajili ya watu wa Sudan Kusini. Rasilimali hii inayohitajika sana itatoa ulinzi na misaada ambayo pale wakati inapohitajika zaidi. Lakini hatua hii haitoshi kwani mpango wa kiutu wa Sudan Kusini umefadhiliwa kwa asilimia tatu pekee. "