Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya uharibifu, hazina za kitamaduni zinaweza kukarabatiwa tena: UNESCO

Licha ya uharibifu, hazina za kitamaduni zinaweza kukarabatiwa tena: UNESCO

Licha ya uharibifu wa thamani isiyokadirika wa urithi wa kitamaduni nchini Iraq, maeneo ya kitamaduni yanaweza kukarabatiwa na kurejeshwa katika hali ya awali baada ya migogoro.

Huo ni mtazamo wa mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na Utamaduni kitengo cha maandalizi ya kukabili dharura Bw. Giovanni Boccardi.

Afisa waandamizi wa UNESCO ameyasema hayo baada ya picha za satellite zilizotolewa siku ya Jumanne, zikionyesha uharibifu mkubwa wa nyumba ya utawa wa Kikristo ya mtakatifu Elia yenye umri wa miaka 1400 mjini Mosul, eneo linalodhibitiwa na kikundi cha kigaidi cha Daesh au ISIL.

Maeneo mengi ya urithi mwingi wa dunia ya Palmyra, nchini Syria, yameharibibwa piana wanamgambo wa Daesh mwaka jana.

Bw. Boccardi, anaelezea zaidi kile kinachoweza kuonekana katika picha

(SAUTI YA BOCCARDI)

"Tunafahamu kile tunachoona kwenye picha za setilaiti, paa limeteketezwa kutokana na uharibifu wa karne ya 18. Lakini bado kulikuwa na vyumba vinavyotumika hata leo. Kulikuwa na mishumaa na vitu vingine. Hili ni jengo jingine amabalo liliteketezwa kwa mkusudi kwa misingi ya misimamo miakali ya dini ya kiislamu."