Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ebola yasababisha njaa kwa mamia ya maelfu ya watu: WFP, FAO

Mwanamke mchuuzi wa vyakula katika soko nchini Sierra Leone, moja ya nchi zilizoathirika na ebola.(Picha ya FAO)

Ebola yasababisha njaa kwa mamia ya maelfu ya watu: WFP, FAO

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yameonya kuwa idadi ya watu wanaokabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na janga la Ebola  nchini Guinea, Liberia, Sierra Leone inaweza kufikia watu milioni moja mwezi Machi 2015 iwapo upatikanaji wa chakula hautaboreshwa na hatua muafaka za kulinda uzalishaji wa nafaka na mifugo hazitachukuliwa.

Katika ripoti yao iliyotolewa leo, mashirika hayo lile la Chakula na Kilimo FAO, na lile la Mpango wa Chakula Duniani, WFP yamesema athari za ugonjwa ni kubwa mno katika nchi hizo tatu ambazo tayari zinakabiliana na upungufu mkubwa wa chakula.

Mashirika hayo yamesisitiza kufungwa kwa mpaka, kuwekwa kwa karantini ,upigaji marufuku wa uwindaji na vikwazo vingine vinazui upatikanaji  wa chakula, na kutishia maisha ya watu, vurugu la masoko ya chakula na kuchochea uhaba inayotokana na hasara ya mazao katika maeneo yaliyo na viwango vya juu vya maambukizi ya Ebola.

Alexander Jones ni Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na wafadhili wa FAO.

(Sauti ya Alexander)

"Tunahitaji pia kukumbuka kuwa kuna umuhimu wa kupunguza athari za usalama wa chakula wa janga hili ambalo ni changamoto. Tunahitaji kufikiria kwamba kando na taarifa tulizopokea za afya , hali hii ina athari za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa mamilioni ya watu katika nchi tatu zilizoathiriwa zaidi ambazo ni Guinea Liberia na Sierra Leone".