Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yazindua ripoti ya kuwezesha wanafunzi walemavu kutumia teknolojia ya mawasiliano

UNESCO yazindua ripoti ya kuwezesha wanafunzi walemavu kutumia teknolojia ya mawasiliano

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO limezindua ripoti ya kuwezesha wanafunzi wenye ulemavu kupata fursa ya kutumia teknolojia ya mawasiliano na habari, ICT. Ripoti hiyo imetolewa hii leo ambayo ni siku ya watu wenye ulemavu duniani na imechapishwa katika lugha Sita, ambazo ni kiingereza, kifaransa, kispaniola, kichina, kiarabu, kirusi na kireno.

Ripoti hiyo ni matunda ya mkutano wa siku mbili wa wataalamu ulioandalia wna UNESCO mwezi uliopita kuangalia changamoto na suluhisho la wanafunzi walemavu katika matumizi ya teknolojia ya mawasiliano. George Njogopa na taarifa kamili.

(TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)