Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajira ya watoto sio tuu ukikaji wa haki zao bali sheria za kimataifa

Ajira ya watoto sio tuu ukikaji wa haki zao bali sheria za kimataifa

Wiki hii dunia imeadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto. Tathimini ya Umoja wa Mataifa imebaini kwamba ajira za shurutio na dhuluma za kimapenzi ni mambo ya kuyatilia maanani saana na ni tatizo linaloelekea kwa sugu.

Zaidi ya watoto milioni 215 wanafanya kazi kote duniani huku zaidi ya nusu yao wakipitia hali ngumu zikiwemo dhuluma za kimapenzi nakazi za shuruti.

Mjumbe maalum kuhusu utumwa Gulnara Shahinian amesema kuwa moja ya ajira za watoto zinazotajwa kwa sasa ni pamoja na kwenye migodi ambapo hadi watoto wa umri wa miaka mitatu hufanya kazi.

Shahinian anasema ni lazima serikali zitekeleze majukumu yao ya kulinda na kuwarejesha kwenye maisha ya kawaida waathiriwa wa ajira ya watoto , kuwafikisha mbele ya sheria wahusika na kuliangamiza kabisa tatizo hilo.

Katika mataifa mengi ya Afrika, watoto huajiriwa sana Kama wafanyakazi wa nyumbani, yaani house girls au house boys,ambako wengi wao hukumbwa na dhuluma mbalimbali, zikiwemo dhuluma za ngono. Ungana na Flora Nducha katika makala hii

(MAKALA NA FLORA NDUCHA)