Matumizi ya sheria yanaweza kumaliza dhuluma dhidi ya wanawake:Manjoo
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Rashida Manjoo ametoa wito kwa serikali ya Papua New Guinea kutumia njia za kisheria kwenye harakati zake za kumaliza dhuluma dhidi ya wanawake.
Akikamilisha ziara yake nchini humo Bi Manjoo pia ameushauri utawala wa nchi hiyo kuondoa baadhi ya itikadi za kitamaduni zinazowadhulumu wanawake.
Mtaalamu huyo amelitwika jukumu na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchunguza dhuluma dhidi ya wanawake, kinachosababisha dhuluma hizo pamoja na athari zake.
Manjoo amesema kuwa wajibu wa kuzuia dhuluma dhidi ya wanawake, kuwalipa fidia waathiriwa na kuwachukulia hatua wahusika uko mikononi mwa nchi.
Kulingana na mtaalamu huyo dhuluma dhidi ya wanawake huanza kutoka nyumbani ambapo watoto wasichana na wanawake hujipata kwenye dhuluma za kimwili na kimapenzi.