Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wapalestina wapatane na Israel kwanza kabla ya kupata taifa:Netanyahu

Wapalestina wapatane na Israel kwanza kabla ya kupata taifa:Netanyahu

Wapalestina wametakiwa kuafikiana amani kwanza na Israel kabla ya kupewa taifa huru. Wito huo umetolewa na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika hotuba yake kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo Ijumaa.

Awali Rais wa Palestina Mahmoud Abbas aliwasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuomba kuwa nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa. Waziri Netanyahu ameliambia Baraza Kuu kwamba kuna silaha yakiwemo maelfu ya makombora Gaza ambayo ni tishio kubwa kwa usalama wa Israel.

(SAUTI YA BENJAMIN NETANYAHU)

Vitisho vyote hivi kwa usalama wa Israel lazima vishughulikiwe kwa muafaka wa amani kabla ya kutangazwa kwa taifa huru kwa sababu tukiyaacha hadi baadaye hayatoshughulikiwa na yatatulipukia usoni na kuvuruga amani. Wapalestina lazima kwanza watakiane amani na Israel kabla ya kupata taifa lao.