Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atoa wito wa kutokuwepo na ghasia na kuheshimu haki za binadamu wakati maandamano yakiendelea Misri

Ban atoa wito wa kutokuwepo na ghasia na kuheshimu haki za binadamu wakati maandamano yakiendelea Misri

Umoja wa Mataifa umeelezea hofu yake kuhusu hali inavyobadilika haraka nchini Misri.

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Maelfu kwa maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana mitaani katika siku ya saba mfululizo kwenye miji mikubwa yote ya nchi hiyo wakimtaka Rais Hossin Mubarak kuachia madaraka.

Waandamanaji hao wanasema kwa miaka 30 aliyokuwa madarakani Rais Mubarak watu wanakabiliwa na matatizo makubwa ikiwemo ukosefu wa ajira, kutokuwepo na uhuru na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon amesema ni muhimu sauti za watu zikasikilizwa na viongozi kutimiza wajibu wao, na watu hao wana haki ya kujieleza, kukusanyika na kuandamana kwa amani.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)