Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM:zaidi ya watu milioni 3 wathirika na tetemeko Haiti

UM:zaidi ya watu milioni 3 wathirika na tetemeko Haiti

Akionekana na huzuni alipokua anazungumza na waandishi habari katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema zaidi ya watumishi 100 wa umoja wa mataifa hawajulikani walipo huko Haiti, na umoja huo unatathmini maafa na hasara zilizopatikana kutokana na tetemeko kubwa la ardhi jana jioni nchini humo.

Katibu mkuu amesema anamtuma mara moja afisa wa cheo cha juu huko Haiti na kutoa dola milioni 10 za msaada wa dharura.

Mkuu huyo wa umoja wa mataifa alisema tetemeko la ardhi limeharibu kabisa mji mkuu wa Port-au-Prince, lakini maeneo mengine ya nchi inaonekana haijathirika. Huduma msingi kama vile maji na umeme katika mji mkuu zimesita kabisa:                             

"Hadi hivi sasa hatujajua idadi ya walofariki au kujeruhiwa, idadi ambayo tunahisi inaweza kuua mamia ya watu. Vituo vya afya vimejaa walojeruhiwa. Hakuna shaka tunakabiliwa na maafa makubwa ya dharura na kutahitajika juhudi kubwa ya huduma za dharura."                                                                                                                                                   

Umoja wa mataifa unazaidi ya walinda amani na polisi elfu 9 huko Haiti, pamoja na watumishi wa kiraia 1900. Makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika hoteli Christopher iliporomoka jana, lakini makao ya vyombo vyake muhimu haikuharibika hata kidogo. Umoja huo unahofia wafanyakazi wake ambao hawajulikani walipo hadi hivi sasa huwenda wamenaswa ndani ya vifusi vya hoteli.

Bw Ban hakuthibitisha vifo vya walinda amani 15 walofariki kutokana na tetemeko akisema kuna wenzao wengi ambao hawajulikani waliko. Miongoni mwao ni mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Haiti afisa wa muda mrefu Hedi Annabi.

Mkuu wa kulinda amani Alain Leroy anasema Umoja wa Mataifa unafanyakazi kujaribu kujua hatima ya wafanyakazi wake wote.

Act Leroy as we speak there are still

Tunapozungumza kungali watu 100 hawajulikani walipo ndani ya vifusi. Kujibu suali lako baadhi ya watu wameokolewa kutoka jingo lakini si zaidi ya 10. Baadhi wamefariki wengine wamejeruhiwa. Kwa hivyo hatujui kwa hivi sasa hatima ya wengine.

Huko Haiti raia walionekana walipanga maiti ziliopatikana kandokando ya barabara, na shirika la msalaba mwekundu huko geneva linasema takriban watu milioni 3 wameathirika na tetemeko hilo kubwa. Shirika hilo la huduma linasema kunahitajika kwa haraka watu watakoajitolea kufanya kazi za uwokozi na hospitali na vituo vya afya vya dharura pamoja na mfumo mpya wa kusafisha maji na kurudisha mawasiliano.