Mataifa ya dunia kusaidia Haiti

Mataifa ya dunia kusaidia Haiti

Marekani na mataifa mengi ya kigeni yameshaanza kupeleka msaada wa dharura huko Haiti, Rais Barack Obama ameahidi mpango kabambe wa dharura ukatayo ratibiwa vyema kusaidia Haiti.

Akizungumza Ijumatano alisema, timu za dharura kutoka marekani ziko njiani kuelekea Haiti, akisema picha za kutoka Haiti ni za kusikitisha sana: "Watu wa Haiti watapata uungaji mkono kamili wa Marekani kwa haraka kabisa kuwaokoa walonaswa ndani ya vifusi na tutawasilisha huduma za dharura chakula maji na madawa, watakaohitaji wa Haiti mnamo siku zinazokuja."


Alisema tume za uwokozi zimeshaondoka na msaada zaidi uko njiani. Na alieleza bayana hakuna wakati wa kupoteza hivi sasa, Ufaransa, Italia, Uingereza na Brazil pia zimeanza kupeleka timu za waokozi na wasaidizi. Idara ya chakula duniani WFP imesema, inasafirisha kwa ndege chakula kutoka ghala zake huko El Salvador, msaada huo unaweza kuwapatia zaidi ya watu nusu milioni chakula.