UNEP kuanzisha mafunzo ya kimtandao kuhusu ulinzi wa mazingira ya asili
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP limeanzisha mafunzo ya kimtandao kuhusu ulinzi wa mazingira ikiwa ni hatua muhimu katika kukomesha migogoro juu ya rasilimali za asili ambayo ni changamoto kubwa katika siasa ya karne ya 21 na kuhatarisha usalama wa binadamu.
Hiyo ni mujibu wa Erik Solheim said ambaye ni mkurungezi wa UNEP katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuzuia vita ambavyo ni sababu kubwa na uharibifu wa mazingira duniani hapo jana tarehe 5 novemba.
Bwana Erik amesema asilimia 40 ya migogoro yote katika kipindi cha miaka 65 iliyopita imechanigia sana uharibifu wa rasilimali za asili. Amesema tangu mwaka 1989, makundi ya wanamgambo zaidi ya 35 yamefadhiliwa na mapato kutokana na rasilimali zitokazo kwenye maeneo yenye migogoro.
Aidha UNEP na baadhi ya vyo vikuu kama chuo Kikuu cha Columbia, chuo kikuu cha Duke, na Chuo Kikuu cha California huko Irvine wameazisha kozi mpya ya kimtandao ya wiki 10 yenye lengo la kutoa mafunzo kuhusu usalama wa mazingira na rasilimali za asili na kudumisha amani katika maeneo yenye migogoro.