Bei za vyakula masokoni zimezidi kupanda kila uchao-Burundi
Pakua
Wakati Ulimwengu ukichagiza uwekezaji zaidi kwenye chakula na maendeleo ya vijijini ili kukabiliana na njaa, hata hivyo katika baadhi ya maeneo watu wameendelea kulalamikia uhaba mkubwa wa chakula.
Nchini Burundi , siku ya chakula duniani imeadhimihswa wakati bei za vyakula masokoni zimezidi kupanda kila uchao.
Mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani KIBUGA makuu ametembelea soko moja la mjini Bujumbura na kutuandalia taaarifa hii.