Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

India: Madhila ya wafanayakazi wahamiaji, UN yataka mshikamano vita dhidi ya COVID-19

Uwepo wa polisi uliongezeka mjini Delhi, India baada ya serikali kutangazwa kufungwa kwa sehemu na shughuli siku 21 kudhibiti COVID-19.
Sandeep Datta
Uwepo wa polisi uliongezeka mjini Delhi, India baada ya serikali kutangazwa kufungwa kwa sehemu na shughuli siku 21 kudhibiti COVID-19.

India: Madhila ya wafanayakazi wahamiaji, UN yataka mshikamano vita dhidi ya COVID-19

Haki za binadamu

Changamoto onevu zinasalia kwa mamia ya maelfu ya wafanyikazi wahamiaji nchini India ambao maisha yao yalisambaratika kufuatia kufungwa kwa ghafla shughuli nchini kote, kufuatia tishio la janga la virusi vya corona, amesema Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Alhamisi.

Bi. Michelle Bachelet kupitia taarifa yake ameelezea kusikitishwa na changamoto za wafanyikazi wa kazi zisizo rasmi walioathiriwa, ambao wengi wao, kwa kulazimishwa, walilazimika kuondoka katika miji ambayo walifanya kazi kwa ilani ya saa chache tu bila uwezo wa kulipa kodi au chakula.
Taarifa ya kamishna mkuu imemnukuu akisema, "ufungiwaji nchini India unazua changamoto kubwa ya utekelezaji kwa kuzingatia idadi ya watu na tunatumai kwamba kuenea kwa virusi kunaweza kudhibitiwa."
Wakati akikaribisha hatua za kushughulikia janga hilo, bi. Bachelet amezingatia umuhimu wa kuhakikisha kuwa hatua zinazochukuliwa kukabiliana na COVID-19 "hazitatumika kwa njia ya kibaguzi au kuzidisha usawa uliopo na udhaifu."
Ukosefu wa kazi na pesa na usafirishaji wa umma kufungwa, mamia ya maelfu ya wahamiaji ambao hawana usalama wa kazi au ulinzi, walilazimika kusafiri mamia ya maili kurudi kwenye vijiji vyao huku wengine wakifariki wakati wa safari, imebaini OHCHR.

Tweet URL

Juhudi za karantini

 

 

Ili kujaribu kudhibiti virusi hivyo, Jumapili, Wizara ya Mambo ya Ndani iliamuru majimbo kuwatenga na kuwaweka chini ya karantini wahamiaji hao kwa wiki mbili.
Hatahivyo, mapema wiki hii, ripoti na picha ziliibuka za maafisa wa polisi wakiwapiga watu ikiwemo wahamiaji kwa kukiuka sheria za karantini na madai ya kunyunyizia watu barabarani, na dawa ya kuua viuatilifu.
"Tunaelewa shida katika huduma za polisi kwa wakati huu, lakini maafisa lazima waonyeshe na kudhibiti viwango vya kimataifa juu ya utumiaji wa nguvu na ubinadamu katika juhudi zao za kukabiliana na janga hili", amesema Bachelet.
Mataifa kadhaa sasa yameamuru polisi waziwazi kuacha kutumia nguvu katika juhudi za kudhibiti kuenea kwa virusi.

 

 

Wahamiaji nao waheshimiwe


Kamishna Mkuu amekaribisha maagizo ya Mahakama Kuu ya India mnamo Jumanne yakisisitiza kwamba wahamiaji hao wanapaswa kuchukuliwa kwa njia ya kibinadamu, pamoja na kuwapa chakula cha kutosha, maji, vitanda na vifaa pamoja na ushauri wa kisaikolojia katika makazi ambayo yanaendeshwa na watu wa kujitolea na sio. vikosi vya usalama.
"Agizo la Mahakama Kuu na utekelezaji wake litachangia katika kuhakikisha usalama na haki za wahamiaji hawa walio katika mazingira magumu", Bi Bachelet amesema. Na kuongeza kuwa,  "Maisha ya watu hawa yamesambaratishwa ghafla na usitishaji wa shughuli na kuwaweka katika hali mbaya sana".
Serikali pia imechukua hatua zingine kushughulikia janga hilo, kwa mfano kusambaza chakula kwa kiwango kikubwa na kushinikiza waajiri kulipa mishahara na wamiliki wa nyumba kutodai kodi.
"Licha ya juhudi hizi zote muhimu, mengi zaidi yanahitaji kufanywa wakati janga la kibinadamu linaendelea kujitokeza mbele ya macho yetu," amesisitiza Kamishna Mkuu.
Ameongeza kwamba hatua maalum zinapaswa pia kuzingatia hali ya wanawake wahamiaji, ambao ni kati ya wale walio katika mazingira magumu zaidi ya kiuchumi na walioathiriwa na hali hiyo.


Sitisha unyanyapaa


Bi Bachelet amesema pia anatiwa wasiwasi na hatua za kudhibiti mlipuko wa corona ambazo zinaathari za kusababisha unyanyapaa kwa sehemu ya jamii kwa mfano kuweka muhuri kwa waliowekwa chini ya karantini ili  kuhakikisha kuwa wanakaa nyumbani, na kuweka ilani nje ya makazi ya watu waliopata karantini.
"Ni muhimu kuzingatia hatua hizo dhidi ya haki ya faragha na kuepuka hatua zinazoweza kuwanyanyasa watu katika jamii, ambao wanaweza kuwa tayari hatarini  kwa sababu ya hali yao ya kijamii au sababu zingine", amesema Kamishna Mkuu.
Kudhibiti wa virusi vya corona au COVID-19 katika nchi ambayo inachukua sudusi moja ya idadi ya watu ulimwenguni itahitaji juhudi sio tu za serikali, bali pia za watu kwa jumla.
Kamishna Mkuu amehimiza serikali kufanya kazi bega kwa bega na vyama vya raia juu ya kushughulikia janga, pamoja na mashirika mengi yasiyokuwa ya kiserikali ambayo tayari yanatoa misaada.
"Huu ni wakati wa mshikamano wa ndani na umoja. Ninahimiza Serikali ishirikiane na vyama vya raia wa India ifikie katika sekta zilizo hatarini zaidi, kuhakikisha kuwa hakuna mtu atakayebaki nyuma wakati huu wa shida ", alihitimisha Kamishna Mkuu.