Ripoti mpya iliyotolewa leo na shjirika la kazi duniani ILO inakadiria kwamba kati ya mwaka 2017 na 2019 idadi ya wahamiaji wa kimataifa imeongezeka kutoka milioni 164 hadi milioni 169, sanjari na kuongeza idadi ya wafanyakazi wahamiaji.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo “Makadirio ya kimataifa ya ILO kuhusu wafanyakazi wahamiaji:matokeo na mfumo” inaonyesha kwamba mwaka 2019 wanayakazi wahamiaji wa kimataifa walikuwa karibu asilimia 5 wa wafanyakazi wote duniani na kuwafanya kuwa chachu muhimu ya uchumi wa dunia.