Mashujaa watanzania wawili miongoni mwa waliotunukiwa medali ya Dag Hammarskjold
Kuelekea siku ya kimataifa ya walinda amani ambayo itaadhimishwa Jumapili hii tarehe 29 Mei, Umoja wa Mataifa umetoa medali kuwatambua na kuwaenzi walinda amani majasiri. Miongoni mwa medali zilizotolewa ni ya Dag Hammarskjoldna kati ya waliotunukiwa ni askari wawili wa Tanzania waliouawa mwaka 2021 wakiwa katika majukumu ya ulinzi wa amani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC.