Mchoro wa kihistoria wa Picasso unaofahamika kama Guernica warejeshwa UN
Mchoro wa kihistoria unaofahamika kama Guernica uliofumwa vizuri kwa nyuzi katika kitambaa kikubwa ukilenga kupinga vita na matukio yake, umerejeshwa tena katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa baada ya kuondolewa takribani mwaka mmoja uliopita ili usafishwe kitaalamu chini ya familia ya mfanyabiashara na mwanasiasa wa zamani wa Marekani, Marehemu Nelson Rockeffeler.