UNMISS na wadau wafungua nyumba salama kwa waathirika wa unyanyasaji wa kingono
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwakushirikiana na wadau wake wamefungua nyumba salama huko Andari Magharibi katika jimbo la Equatoria kwa ajili ya kusaidia manusura wa unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro nchini humo.