UNMISS yaendesha doria Tambura kufuatia maelfu ya watu kuyakimbia makazi yao
Kufuatia kuuawa kwa watu kadhaa na zaid ya watu elfu themanini kuyakimbia makazi yao katika kipindi cha miezi sita iliyopita jimboni Tambura nchini Sudan Kusini Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNMISS unaendesha doria za mara kwa mara jimboni hapo huku ukitoa ulinzi kwa maelfu ya raia walioyakimbia makazi yao.